IAEA yaanzisha uchunguzi baada ya Marekani kushambulia kituo cha nyuklia Iran
Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limetangaza kuwa linafanya uchunguzi kuhusu taarifa za shambulio la usiku wa kuamkia leo dhidi ya eneo ambalo kiwanda cha nyuklia cha Darkhovin, kilikuwa kinajegwa nchini Iran.
Shirika hilo limesema kituo hicho kilikuwa bado katika hatua za kwanza za ujenzi, na walipofanya ukaguzi wao wa mwisho, hakukuwa na nyenzo za nyuklia zilizokuwepo katika eneo hilo.
Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran limeshutumu Marekani kwa kushambulia kituo kilichokuwa kikijengwa cha nyuklia cha Darkhovin.
Katika taarifa yake, shirika hilo limesema kuwa Marekani, imekiuka sheria za kimataifa kwa kushambulia kituo hicho.
Soma pia: