Zaidi ya wanajeshi 50 wauawa na kundi la waasi nchini Mali

Chanzo cha picha, Getty Images
Wapiganaji wa waasi wa Tuareg nchini Mali kwa kushirikiana na wanamgambo wengine wenye itikadi kali, wamevamia msafara wa jeshi la Mali katika eneo la Gao, na kuua angalau wanajeshi 50, kulingana na maafisa waliozungumza na shirika la habari la AFP.
Kwa kujibu shambulio hilo,jeshi la Mali limesema lilitekeleza mashambulizi ya anga yaliyowalenga wapiganaji hao na kuwaua takriban wapiganaji 20, kuharibu magari manne ya kubeba wapiganaji na kuangamiza ngome tatu za waasi karibu na eneo la Tabrichat, hatua iliyowezesha msafara wa jeshi hilo la Mali kuendelea na safari yake.
Hata hivyo, maafisa wameiambia AFP kuwa idadi ya waliouawa ni zaidi ya wanajeshi 50, huku angalau wanajeshi 24 wakidaiwa kutekwa na waasi hao, na kufanya hili kuwa moja ya mashambulizi mabaya zaidi dhidi ya jeshi la Mali katika miaka ya karibuni.
Kundi la The Azawad liberation front, linaloshirikiana na kundi la wanamgambo la JNIM, limedai kuhusika na shambulio hilo, ilamadai hayo hayajathibitishwa.
Kwa sasa hali ya usalama kaskazini mwa Mali inazidi kuwa tete, polisi wakikabiliana na makundi ya waasi wenye itikadi kali.
Soma pia:










