Tetesi za soka Ulaya Ijumaa: Inter Milan wanasuka mipango kumsajili Spence

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 1

Inter Milan wanania ya kumsajili Djed Spence na Cristian Romero, Liverpool wanaongoza mbio za kumsajili Kaishu Sano, huku Arsenal wakimwania Ezri Konsa.

Inter Milan wanasuka mipango ya kumsajili beki wa pembeni wa Tottenham na England, Djed Spence, 25, pamoja na beki wa kati wa Argentina, Cristian Romero, 28. (Corriere dello Sport - in Italian)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool wanaongoza mbio za kumsajili kiungo wa Japan, Kaishu Sano, kutoka Mainz na wako tayari kutoa hadi euro milioni 60 (£50.9m) kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye pia anawindwa na Arsenal, Tottenham na Borussia Dortmund. (Teamtalk)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal wameonyesha nia ya kumsajili beki wa Aston Villa na England, Ezri Konsa, mwenye umri wa miaka 28. (Guardian)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kipa wa Crystal Palace na Argentina, Walter Benitez, mwenye umri wa miaka 33, anaweza kuvunja mkataba wake na Palace ili kurejea Nice. (Nice-Matin - in French)

Liverpool wamewasiliana na Bournemouth kuhusu winga wa miaka 19, Rayan, wakilenga kumrejesha Mbrazil huyo chini ya kocha wao wa zamani, Andoni Iraola. (Teamtalk)